Kwa upande wa usomaji au qiraa , Waheed Wakili alikuwa mshindi wa kwanza na Hashim Sultani Nejad aliibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa hifdh. Taarifa zinasema kuwa, kwa upande wa usomaji nafasi ya pili hadi ya tano zilishikwa na wasomi Abdul Rahman al Kurdi wa Syria, Saeed Barat Zadeh kutoka Ujerumani, Muhammad Ali Khosrawi wa Afghanistan na Hissam Karim kutoka Iraq. Kwa upande wa hifdh, nafasi ya pili hadi ya tano ilikuwa katika utaratibu ufuatao; Saidu Adam Is haq kutoka Nigeria, Hussein Adnan AbdulRazzaq kutoka Iraq, Muhammad Irshad bin Abdullah kutoka Malaysia, Sayyid Sadiq Ehsani kutoka Afghanistan. Duru ya 30 ya mashindano ya kimataifa ya Qurani Tukufu ilianza tarehe 31 Mei kwa kuwashirikisha wasomaji na mahafidh kutoka nchi 75 duniani.
1238887