IQNA

'Uchaguzi Iran unainua uwezo wa taifa kimataifa'

21:56 - June 14, 2013
Habari ID: 2546956
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran, Ayatullah Muhammad Imami Kashani amesema kuwa, kufanyika uchaguzi uliofana kwa kushiriki wananchi wengi, kunainua uwezo na maendeleo makubwa ya mfumo wa Kiislamu ndani ya Iran na katika nyuga mbalimbali za kimataifa.
Ayatullah Kashani ameitaja siku ya leo kuwa siku ya kipekee na muhimu zaidi kwa wananchi na mfumo wa Kiislamu wa Iran na kwamba, kujitokeza kwa wingi ya wananchi katika masanduku ya kupigia kura, kwa hakika kutainua nafasi ya taifa hili duniani. Amesema kadri uchaguzi wa rais na wa mabaraza ya miji na vijiji utakavyohudhuriwa na wapiga kura wengi ndivyo hivyo hivyo utakavyoinua uwezo na heshima ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hususan mbele ya maadui na vibaraka wasiolitakia mema taifa hili. Aidha Khatibu wa Sala ya Ijumaa amewahutubu wagombea wa urais akiwaambia kuwa, katika uchaguzi huu hakuna atakayeshindwa na kwamba jambo muhimu ni kuwa, ushindani huu unatakiwa uwe sababu ya kuleta maelewano na umoja wa taifa la Iran na kwamba, huo ndio ushindi wa wagombea wote. Hii ni katika hali ambayo hadi tunaandika habari hii upigaji kura unaendelea na muda wake umeshaongezwa mara mbili, mara ya kwanza kwa muda wa masaa mawili na mara ya pili kwa muda wa saa moja.
1242472
captcha