IQNA

Iran yalaani mazunguzmo ya Marekani na Taliban nchini Qatar

10:57 - June 23, 2013
Habari ID: 2550979
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Abbas Araqchi amesema Tehran inapinga mazungumzo ya Markekani na wanamgambo wa Taliban huko Doha, mji mkuu wa Qatar.
Akizungumza Jumamosi, Araqchi amesema kuwa mazungumzo ya kulazimishwa yanayoongozwa na madola ya kigeni yanakiuka maslahi ya kitaifa ya Afghanistan. Amesema mazungumzo hayo hayawezi kuwa na natija nzuri kwani yanafanyika pasina kuwepo wawakilishi halisi wa taifa la Afghanistan.

Mwakilishi maalumu wa Marekani nchini Afghanistan na Pakistan James Dobbins tayari yuko mjini Doha kwa lengo la kuongoza mazungumzo na Taliban. Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amesema serikali yake haitashiriki katika mazungumzo yoyote baina ya Marekani na Taliban hadi pale mazungumzo hayo yatakapoongozwa na Waafghan wenyewe.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Afghanistan imetoa taarifa ikibainisha kuchukizwa kwake na hatua ya kundi la Taliban kupewa idhini ya kufungua ofisi nchini Qatar.
1246837
captcha