IQNA

Imam Khamenei aisifu serikali ya rais Ahmadinejad

15:34 - July 15, 2013
Habari ID: 2561928
Katika siku ya tano ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, Ayatullahil Udhma Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, amekutana na Rais Mahmoud Ahmadinejad pamoja na baraza lake la mawaziri, na kusifu kazi na juhudi zake kubwa za usiku na mchana katika kuhudumia taifa na kudumisha kaulimbiu ya mapinduzi katika nyuga mbalimbali, ndani na nje ya nchi.
Kiongozi Muadhamu Sayyid Ali Khamenei ameshiria njama za baadhi ya wapinzani wa ndani na nje na vyombo vya habari vya kigeni katika kufumbia macho juhudi kubwa za serikali na kusema, katika miaka minane ya hivi karibuni, kila mtu amehisi na kudiriki kuwa Rais na baraza lake la mawaziri sambamba na kukabiliwa na changamoto chungu nzima, wamefanya kazi kubwa kuliko serikali zote zilizotangulia. Aidha kiongozi Muadhamu, ametaja mipango ya kuimarisha kaulimbiu za Mapinduzi kuwa ni jambo la dharura na kuongeza kuwa, mrengo ulio dhidi ya Mapinduzi umefanya njama nyingi zenye lengo la kupotosha kaulimbiu hizo na ikiwezekana kuzifuta kabisa taratibu. Aidha amesema njama hizo zimefeli kutokana na uelewa mkubwa wa Imam Khomein (MA) katika kuzidumisha kaulimbiu hizo. Kwa upande mwingine, Kiongozi Muadhamu, ameusia kutekelezwa wajibu na kuacha mambo yaliyoharamishwa na sheria za Kiislamu ili kuweza kuvuka kwa amani njia hii ya dunia kuelekea Kiama. Mwishoni mwa kikao hicho ambacho ni cha mwisho cha Rais Mahmoud Ahmadinejad na Baraza lake la Mawaziri na Kiongozi Muadhamu, maafisa hao wa serikali walitunukiwa zawadi ya nakala za Qur’ani Tukufu kutoka kwa Kiongozi Muadhamu.
1257915
captcha