Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vijavyo kwanza unapaswa kufikia hatima ya miji ya utawala huo ghasibu kabla ya kuishambulia Bairut, na kusisitiza kwamba Israel haina ubavu tena wa kuikalia kwa mabavu ardhi ya Lebanon.