Akizungumza Jumatano bungeni, Larijani alisema wabunge wa Iran wanalaani vikali hatua hiyo ya kuchukiza ya Umoja wa Ulaya na kuitaja kuwa ni ya kisiasa. Ikumbukwe kuwa Julai 22, chini ya mashinikizo ya Marekani na utawala haramu wa Israel, Umoja wa Ulaya uliamua kuliwekea vikwazo tawi la kijeshi la Hizbullah.
Spika wa Majlisi ya Iran amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuunga mkono kikamilifu harakati ya Hizbullah ya Lebanon. Larijani ameongeza kuwa uamuzi wa Umoja wa Ulaya unatokana na kuwa Hizbullah imekuwa ikiwalinda watu wa Lebanon ambao wanakabiliwa na uhasama mkubwa wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Larijani aliashiria ushindi wa Hizbullah dhidi ya Israel katika vita vya siku 33 mwaka 2006 na kusema, ushindi kama huo umezitia wasi wasi nchi za Magharibi.
Shakhsia mbalimbali diniani wameendelea kuonesha upinzani wao mkubwa dhidi ya uamuzi wa Umoja wa Ulaya (EU) wa kuiweka harakati ya Hizbullah katika orosha yake ya makundi ya kigaidi.
Radiamali kali ya fikra za waliowengi nchini Lebanon, katika nchi za Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya uamuzi huo wa Umoja wa Ulaya imeonesha kuwa, watu hao hawakuathiriwa na propaganda chafu za utawala wa Kizayuni wa Israel na witifaki wake. Si hayo tu, bali hatua hiyo ya Umoja wa Ulaya itazidisha chuki na hasira za waliowengi katika Mashariki ya Kati na kwenye Umma wa Kiislamu dhidi ya umoja huo.
Hapana shaka kuwa, kufeli kwa utawala wa Kizayuni na mafanikio ya mara kwa mara ya Hizbullah yameutia wasiwasi mkubwa utawala ghasibu wa Israel na waitifaki wake wa Kimagharibi.
Katika hali kama hiyo Israel na nchi hizo za Ulaya zimeamua kuchukua hatua kama hizo za kuiweka Hizbullah katika makundi eti ya kigaidi ili kuficha kushidwa kwa utawala huo haramu kwa upande mmoja, na kulipiza kisasi dhidi ya wanamapambano wa Hizbullah katika upande wa pili. Hii ni pamoja na kuwa, kwa hatua hiyo, Umoja wa Ulaya unataka kuzipotosha fikra za walimwengu kuhusu sura na hakika ya kigaidi ya Israel na kuhusu misaada yake kwa makundi mbalimbali ya kigaidi ya Mashariki ya Kati hususan huko Syria.
Alaa Kulli hal, Hizbullah imethibitisha kuwa, daima umekuwa ngome imara mbele ya chokochoko zote za utawala ghasibu wa Israel na vitimbi vya nchi za Magharibi ambazo zimetambua kuwa, wanamapambano wa Hizbullah ni kisiki kikubwa kinachokwamisha malengo yao machafu katika eneo hili.
1263004