Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei alisema hayo jana jioni wakati alipoonana na wanachuo na wawakilishi wa asasi za kielimu, kiutamaduni, kisiasa n.k, za Vyuo Vikuu vyote vya Iran na kusisitiza kuwa, matukio yanayoendelea kushuhudiwa hivi sasa Misri yanaonesha kina na kilindi kirefu cha mwamko wa Kiislamu nchini humo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pia kuwa, mwamko wa Kiislamu haukuongozwa vizuri nchini Misri na kusisitiza kuwa, yanayotokea nchini Misri hivi sasa yanahuzunisha na kuumiza sana na hayo yote ni kutokana na kufanyika makosa katika kuongoza mwamko huo wa Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mwamko wa Kiislamu ni tukio muhimu ambalo haliwezi kufutika kutokana na hoja zisizo za kimatiki za ubeberu.
Amesema kutokana na kukosekana tadbiri nzuri ya mwamko huo leo taifa la Misri linashuhudia hali mbaya na ya kusikitisha kote ulimwenguni.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, ikiwa mirengo na jumuiya za wanafunzi zitafanya utafiti wa kina kuhusiana na mwenendo wa mwamko wa Kiislamu na hofu ya uistikbari katika kukabiliana na tukio hilo pamoja na makosa yaliyotendeka katika nchi za eneo kuhusiana na tukio hilo, zitakuwa zinahudumia taifa lao.
Aidha sambamba na kubainisha stratijia ya kina ya mfumo wa Kiislamu, Kiongozi Muadhamu amesema kuwa, kwa kutazama mambo kwa uhalisia wake kuhusiana na matukio ya Mashariki ya Kati inafahamika wazi kwamba, baadhi ya mambo ni chimbuko la kuzidi kupata nguvu mfumo wa Kiislamu na kwamba ni ishara ya wazi kuwa, stratijia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni ya kutazama na kuzingatia mambo kwa kina zaidi.
1265290