Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo katika ujumbe wake kwa 'Kongamano la 22 la Kitaifa la Sala'. Katika ujumbe wake huo, amesema maana ya kuboreshwa kiwango cha sala ni kuhakikisha kuwa sala inasimamishwa kwa mahudhurio ya moyo na mwenye kusali aitazame sala kama 'mkutano wake na Allah'.
AIdha katika ujumbe wake Kiongozi Muadhamu alisisitiza umuhimu wa kujengwa maeneo ya kusalia katika sehemu za umma kama vile viwanja vya michezo, mabustani na vituo vya mabasi. Aidha aliwataka wenye vyombo vya kusafiria kuzingatia wakati wa sala.
Kongamano hilo la Kitaifa la Sala ambalo lilianza jana Jumatano katika Chuo Kikuu cha Lorestan magharibi mwa Iran limehudhuriwa na idadi kubwa ya wanazuoni na maulamaa.
Akizungumza katika kikao hicho, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran au bunge Dkt. Ali Larijani aliashiria umuhimu wa Madrassa za Kiislamu na Misikiti kwa kusema: "Lengo la Madrassah za Kidini na Misikiti ni kulinda dini ya watu na hili ndio suala muhimu zaidi katika maisha ya mwanaadamu…..kutokana na uzoefu wangu , iwapo mji utakuwa na madrassah na misikiti yenye kufanya kazi ipasavyo basi mji huo utakuwa ni wenye utamaduni mzuri."
1282458