IQNA

Larijani: Matokeo ya vita Syria hayatabiriki

8:09 - September 08, 2013
Habari ID: 2585954
Spika wa Bunge la Iran Ali Larijani ameonya kuhusu vita tarajiwa vya Marekani dhidi ya Syria na kusema natija ya vita hivyo haiwezi kutabirika.
Akizungumza mbele ya Bunge la Turkmenistan siku ya Ijumaa, Larijani amesema Iran inapinga vikali vita dhidi ya Syria na kuongeza kuwa marekebisho ya kisiasa hayawezi kufanyika katika nchi hiyo ya Kiarabu kwa mtutu wa bunduki na ugaidi.
Wakati huo huo Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu Iran Ayatullah Hashemi Rafsanjani amelaani vikali vitisho vya Marekani dhidi ya Syria. Akizungumza jana Jumamosi, Larijani alielezea wasi wasi wake kuhusu kuongezeka vitisho vya kijeshi dhidi ya Syria. Amesema dola lenye kiburi la Marekani linataka kuzidhibiti nchi za Kiislamu.
Marekani na waitifaki wake wachache wanapanga kuivamia kijeshi Syria kwa madai kuwa serikali ya nchi hiyo imetumia silaha za kemikali. Serikali ya Syria imekanusha madai hayo na kusema silaha hizo zimetumiwa na magaidi wanaopata himaya ya Marekani, Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na Utawala haramu wa Israel.
1283512
captcha