IQNA

Nakala kubwa zaidi ya Qur'ani duniani yaandikwa Iran

15:32 - May 05, 2015
Habari ID: 3259424
Nakala kubwa zaidi ya Qur'ani duniani imeandikwa katika mji mtakatifu wa Mash'had kaskazini maashariki mwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mkuu wa kitengo cha Qur'ani na Itra Katika idara ya Wizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu  Iran katika mkoa wa Khorassan Razavi, Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammad Taqi Kadhiminasab amesema nakala hiyo yenye thamani kubwa ina uzito wa kilo 5.3 na kurasa 650 na inatambuliwa kuwa Qur'ani kubwa zaidi iliyoandikwa kwa hati za mkono duniani.


Kadhiminasab amongeza kuwa, nakala hiyo kubwa zaidi ya Qur'ani duniani imeandikwa na Ustadh Ali Akbar Ismaili Quchani, na wasanii 30 wa kike wamefanya kazi ya kuipamba na kuinakishi kwa maji ya dhahabu. Amesema kila juzu moja ya nakala hiyo ya Qur'ani imeandikwa kwenye kurasa 20 na kwamba karatasi za nakala hiyo ya Qur'ani zimetengenezwa na kutayarishwa na mwandishi mwenyewe.


Miongoni mwa sifa za nakala hiyo kubwa zaidi ya Qur'ani duniani ni kwamba inaweza kuoshwa kwa maji na haiwezi kupondwapondwa wala kufinyangwa. Vilevile rangi za aya za nakala hiyo ya Qur'ani haziwezi kufutika.../EM

3252580

Kishikizo: qur'ani iran kubwa
captcha