katika mahojiano maalumu na Shirika la Kimataifa la Habari la Qur'an la Iran IQNA, Abdul Majid Ahmed Muhammad al-Hamdan amesema mashindano ya Qur'ani Iran yanatoa mchango mkubwa katika kuimarisha umoja wa Kiislamu hasa kwa kuzingatia hali ya hivi sasa katika ulimwengu wa Kiislamu. Amesisistiza kuwa, umoja, mshikamano na maelewano katika Ummah wa Kiislamu ni nukta muhimu sana katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Iran.
Qarii huyo kutoka Saudi Arabia amesema washiriki katika mashindano ya Qur'ani nchini Iran ni kutoka madhebu yote ya Kiislamu na kilichowaleta pamoja woote ni kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu. Amesema mashindano hayo yanaashiria umoja unaoweza kupatikana katika Ummah wa Kiislamu.
Awamu ya 32 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yalianza Ijumaa Mei 15 (27 Rajab) kwa mnasaba wa kubaathiwa Mtume SAW. Mashindano hayo ya wiki moja yamewaleta pamoja maqarii 120 kutoka nchi 75.../mh