Afisa wa kitengo cha Qur'ani na Itra katika Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu, Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammad Reza Heshmati, amesema maonyesho hayo yatafanyika nyakati za usiku za mwezi wa Ranadhani hapa mjini Tehran na kwamba yatakuwa na ratiba na programu mbalimbali. Amesema maonyesho hayo ya kimataifa ya Qur'ani yatakuwa na vitengo vya watoto na vijana, sanaa na turathi, kitengo cha vyuo vikuu, hijabu na utakasifu, elimu na malezi, maonyesho ya vitabu, wahudumu wa Qur'ani na wanawake na mazingira.
Hujjatul Islam Heshmati ameongeza kuwa maonyesho mengine kama hayo ya Qur'ani ya Tehran yatafanyika pia katika miji 30 hapa nchini katika mwezi wa Ramadhani kwa lengo la kueneza mtindo wa maisha wa Kiislamu.
Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani unatazamiwa kuanza Alkhamisi, Juni 18 hapa nchini Iran na aghalabu ya maeneo mengine duniani.../mh