Naibu Mwenyekiti wa Kongamano la Kimataifa la Uyghur Seyit Tumturk amesema ni jambo la kusiktisha kuwa jamii ya kimataifa imenyamzia kimya kila alichosema ni ukandamizaji wa Waislamu wa China. Akiashiria hatua ya Waislamu kupigwa marufuku kufunga Sawm ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika jimbo la Xinjiang, amesema hilo ndilo eneo pekee duniani ambapo Waislamu wamepigwa marufuku kufunga.
Ameongeza kuwa hii si mara ya kwanza kwa wakuu wa eneo hilo la China kuwazuia Waislamu kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Mwanaharakati huyo amesema kwa muda wa miaka 66 sasa China imekuwa ikitekeleza sera za kuwalazimisha Waislamu wa Xinjiang kuacha dini yao. Aghalabu ya wakaazi wa eneo la Xinjiang ni Waislamu wa kabila la Uighur ambapo, kutokana na sera hizo za kibaguzi na ukandamizaji, kumekuwepo pia na uasi wa wanaotaka kujitenga na kuanzisha nchi huru.../mh