Akizungumza hapo jana alasiri mbele ya Rais Hassan Rouhani na baraza lake la mawaziri, Ayatullahil udhma Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisherehesha na kubainisha sehemu ya maagizo muhimu ya Imam Ali (as) kwa Malik Ashtar, gavana wake huko Misri na kusisitiza kwamba, nguzo ya kiroho, kimaanawi na kifikra ni sababu kuu ya kutatuliwa matatatizo yote na kwamba kuzingatia na kutafakari kwenye Nahjul Balagha, kitabu kinachobeba semi, barua na hotuba za Bwana wa Mutaqeen, Imam Ali (as) kunamwandalia mwanadamu nguzo na ngome madhubuti kama hiyo. Kiongozi Muadhamu ameashiria hotuba ya Rais Rouhani mwanzoni mwa mazungumzo hayo kuhusu natija ya mazungumzo ya nyuklia na madola makuu duniani na kupongeza jitihada, mapambano ya dhati na umakini wa timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amebainisha jukumu la viongozi katika agizo la Amir Muuminin kwa Malik Ashtar na kuongeza kuwa, kuchukua kodi na haki nyingine ambazo serikali inazo kwa wananchi, kuwalinda wananchi na ardhi yao, kuilekeza jamii kwenye mambo mema, maendeleo na ujenzi wa taifa ni majukumu manne ambayo Imam Ali (as) aliyasisitiza kwenye barua ya maagizo aliyomwandikia Malik Ashtar, majukumu ambayo watawala wanapasa kuyatekeleza kwa taifa.
Kiongozi Muadhamu amesema kuwa utendaji mema ndiyo akiba bora zaidi ya kipindi cha uongozi wa kila mtu na kuongeza kuwa wananchi huwa hawakosei katika utoaji maoni uliosimama juu ya msingi wa fikra salama, uzingatiaji na natija iliyodurusiwa vyema na kwamba kwa msingi huo tunaweza kufahamu kutokana na hukumu hiyo ya wananchi ni kiongozi yupi aliye mwema na yupi asiyekuwa mwema.
Uchungaji mkubwa na wa makini wa nafsi na kuizuia isipotee njia pamoja na kufadhilisha taklifu na maamrisho ya Mwenyezi Mungu juu ya kila jambo ni usia mwingine uliotolewa na Kiongozi Muadhamu alipokuwa akibainisha maagizo ya Amir al-Mumineen kwa Malik Ashtar. Alisema hayati Imam Khomeini (MA), mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran alikuwa dhihirisho halisi la utekelezaji wa maagizo hayo matukufu. Mwishoni mwa mazungumzo hayo Kiongozi Muadhamu alilishukuru Baraza la Mawaziri kwa juhudi linazofanya na kulitakia mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yake.
Kabla ya hutoba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais Hassan Rouhani aliashiria matokeo ya hivi karibuni ya mazungumzo ya nyuklia na kumshukuru Kiongozi Muadhamu kwa uungaji mkono na mwongozo wake kwa serikali na timu ya mazungumzo. Ameelezea matumaini yake kwamba jambo hilo litaandaa uwanja wa kukomeshwa mashinikizo na tuhuma zisizofaa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na pia kuanzisha harakati mpya katika njia ya maendeleo na ustawi nchini. Katika kikao hicho Rais Rouhani pia ametoa ripoti kuhusiana na utendaji wa serikali yake...mh