
Mshauri wa mkoa huo, Marouf al-Rifai, alieleza kuwa uchimbaji unaoendelea, ikiwemo mitaro inayounganisha maeneo kadhaa yanayohusiana na makazi ya walowezi , unaweza kudhoofisha ardhi iliyo chini ya Al-Aqsa.
Alisema kuwa shughuli hizo “zinaweza kusababisha uharibifu wa alama muhimu za kihistoria za Wapalestina, kama vile nyumba za kale na shule za zamani, na pia kuathiri udongo ulio chini ya Msikiti wa Al-Aqsa, jambo linalotishia uthabiti wa misingi yake.”
Al-Rifai aliongeza kuwa uchimbaji huo “hauna misingi ya kielimu na unakiuka hali ya sasa ya kidiplomasia (status quo),” akisisitiza kuwa unaendeshwa kwa misingi ya kisiasa.
Aidha, alieleza kuwa majeshi ya uvamizi ya Kizayuni yaliingia katika mji mmoja karibu na Al-Quds na kutoa amri za kubomoa karakana na viwanda vya kutengeneza vyuma na samani.
Alifafanua kuwa maagizo hayo ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kujenga miundombinu mipya, ikiwemo barabara, mzunguko (roundabout), na daraja litakalounganisha makutano ya Anata na kituo cha ukaguzi cha Hizma , na kusema kuwa Wazayuni wanakusudia kuondoa majengo ya Wapalestina yaliyo katika njia ya mradi huo kwa visingizio mbalimbali, kama vile ukosefu wa vibali vya ujenzi na ukaribu wake na ukuta wa utengano.
Kauli ya mkoa huo imetolewa wakati ukiukwaji wa mara kwa mara unaendelea ndani na kuzunguka eneo la Msikiti wa Al-Aqsa. Mapema Alhamisi, makundi ya walowezi wa Kiyahudi walivamia eneo hilo takatifu la Kiislamu wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi na jeshi. Mashuhuda wamesema kuwa makundi hayo yalizunguka eneo hilo kwa zamu.
Katika wiki za hivi karibuni, mamlaka za Kizayuni zimeongeza hatua za kiusalama katika milango na maeneo yanayozunguka Msikiti wa Al-Aqsa, kwa kupeleka maafisa wa ziada ili kulinda uvamizi wa walowezi, kwa mujibu wa ripoti hiyo.
3495126