IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Iran itaendelea kuunga mkono wananchi wa Palestina

18:57 - July 18, 2015
Habari ID: 3329110
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullahil-Udhma Sayyid Ali Khamenei, amesema taifa la Iran litaendelea kuwaunga mkono marafiki zake katika eneo la Mashariki ya Kati kama vile wananchi wa mataifa ya Yemen, Palestina, Bahrain, Iraq, Syria na Lebanon.

Kiongozi Muadhamu, ameyasema hayo leo asubuhi katika hotuba aliyoitoa baada ya sala ya Iddil-Fitr na kusema Iran itaendelea na msimamo huo  sawa sawa matini ya makubaliano ya nyuklia yatapasishwa au la. Aidha ameashiria kadhia ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1, ambapo mbali na kuwasifu wahusika wa mazungumzo hayo marefu na mazito, amesisitiza kuwa, juhudi za timu ya Iran katika mazungumzo hayo, hazipaswi kufumbiwa macho, bila kujali kuwa matini ya mapendekezo ya makubaliano hayo yatapasishwa au la. Amefafanua zaidi kuwa, Iran kamwe haitasalimu amri mbele ya matakwa ya adui kama vile ambavyo haitaruhusu kutiwa doa muundo wa mfumo unaotawala nchini hapa. Kiongozi Muadhamu pia amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kulinda muundo wake wa kiulinzi na kiusalama, hata kama maadui wataendelea kufanya njama zao katika uwanja huo.
Akiashiria tofauti kubwa zilizopo katika siasa za Iran na Marekani katika eneo Ayatullahil-Udhma Sayyid Ali Khamenei  amesema kuwa, Marekani inaituhumu Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon kwa ugaidi, katika hali ambayo ni Marekani hiyo hiyo ndiyo inayounga mkono utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ambao ndio asili ya ugaidi na unaoua watoto na wanawake, na kuhoji kuwa ni vipi siasa hizo zinaweza kuwekwa kwenye meza ya mazungumzo na Iran? Amesisitiza kuwa, tangu mwanzo wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, marais wote watano waliotawala Marekani licha ya kufanya njama mbalimbali za kuishinikiza Iran isalimu amri mbele ya taifa hilo, walishindwa na kwamba, wengine wamekufa wakiliacha taifa la Iran ya Kiislamu likiwa bado katika mkondo wake huo.
Kiongozi Muadhamu ameashiria juu ya migogoro ya eneo, na kusema kuwa mabadiliko yaliyojiri katika eneo ndani ya mwezi wa Ramadhani na kabla yake, yalizifanya kuwa mbaya siku za mwezi Kiongozi Muadhamu amesema kuwa, mikono michafu ya viongozi waovu, iliifanya kuwa chungu Ramadhani ya mwaka huu ya watu wa eneo la Mashariki ya Kati.huo, kwa Waislamu na waumini wa eneo la Mashariki ya Kati.../mh

3329071

captcha