IQNA

Nakala ya kale zaidi ya Qur’ani yagunduliwa Uingereza

20:12 - July 22, 2015
Habari ID: 3332252
Nakala ambayo yumkini ikawa miongoni mwa nakala za zamani zaidi za kitabu kitakatifu cha Qur’ani Tukufu imegundulwia nchini Uingereza.

 Uchunguzi uliofanyika katika ngozi ambayo Qur’ani hiyo imeandikwa  umethibitisha kuwa mnyama wa ngozi hiyo alikuwa akiishi katika zama za Mtume Muhammad (saw) au muda mfupi baadaye.

Prof David Thomas wa Chuo Kikuu cha Birmingham nchini Uingereza ambaye ni mtaalamu wa Uislamu na Ukristo amesema kuwa matokeo ya uchunguzi huo yanashangaza na kwamba nakala hiyo ya Qur’ani ya kale inafanana na Qur’ani iliyopo hivi sasa baina ya Waislamu. Thomas amesema uchunguzi wa Chuo Kikuu cha Oxford, kwa kutumia mionzi Maalum ya carbon ya kutambua vitu vya zamani (Radiocarbon) imethibitisha kuwa asilimia, umebaini kuwa, kuna uwezekano wa asilimia 95 kwamba nakala hiyo iliandikwa baina ya mwaka 568 hadi 645 Miladia na kwa msingi huo mtu aliyeiandika alikuwa akiishi katika zama za Mtume Muhammad (saw).

Profesa huyo amesisitiza kuwa, ugunduzi wa moja kati ya nakala za kale zaidi za Qur’ani umesisimua sana.

Imedokezwa kuwa nakala hiyo ya kale ya Qur'ani ni miongoni mwa maelfu ya nyaraka zingine za kale kutoka mashariki ya kati ambazo zilimilikiwa na mwana historia mzawa wa Iraq, Alphonse Mingana, aliyekabidhi kwa chuo kikuu hicho cha Birmingham mwaka 1920.

Qur'ani hiyo ambayo imeandikwa kwa maandishi ya Hijazi itaonyeshw akwa ummah mwezi Oktoba mwaka huu katika Chuo Kikuu cha Birmingham.../air

 3331972

captcha