IQNA

Mshindi wa Mashindano ya Qur’ani Malaysia apata zawadi ya Kiongozi Muadhamu

12:26 - July 23, 2015
Habari ID: 3332311
Msomaji bora katika Mashindano ya 57 ya Kimatiafa ya Qur’ani Malaysia amepokea zawadi kutoka kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Raia wa Iran Muhsin Hajjhassani Kargar aliibuka mshindi katika kitengo cha qiraa cha mashindano hayo ya Qur’ani yaliyofanyika nchini Malaysia mwezi Juni.
Qarii huyo ametuma katika mtandao wake wa kijamii, Instagram, picha ya pete ya akiki aliyopokea kama zawadi kutoka kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Maquraa na mahufadh kutoka zaidi ya nchi 70 walishiriki katika Mashindano ya 57 ya Kimataifa ya Qur’ani yaliyofanyika Malaysia kuanzia Juni 9.
Hajihassani Kargar alishika nafasi ya kwanza katika qiraa huku wa pili akiwamwakilishi wa Ufilipino akifuatiwa na Mburunei na Mualgeria kwa taratibu.
Katika kuhifadhi Qur’ani  wawakilishi wa Qatar, Kuwati na Tunisia walishika nafasi za kwanza hadi tatu kwa taratibu.
Washiriki wa Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Malaysia wamewashi kushinda mara tisa na kupata nafasi ya pili mara nane.../mh

3331975

captcha