IQNA

Wafanyaziara zaidi ya 107 wafariki, 238 wajeruhiwa kwa kuanguka kreni Makka

23:34 - September 11, 2015
Habari ID: 3361271
Wafanyaziara wasiopungua 107 wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na kreni au winchi katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia.

Duru za Saudia zimeripoti leo kuwa, upepo mkali na kimbunga kimeliangusha chini winchi hilo. Watu wasiopungua 238 wamejeruhiwa katika ajali hiyo.
Kuna uwezekano wahanga wa ajali hiyo wakaongezeka.

Serikali ya Saudi Arabia imekuwa ikitekeleza miradi kadhaa ya kuupanua Msikiti Mkuu wa Makka ambapo miradi hiyo inakadiriwa kugharimu zaidi ya dola bilioni 26.

Ajali ya leo Ijumaa imejiri siku chache tu kabla ya kuanza ibada ya kila mwaka ya Hija.../mh

3361260

captcha