IQNA

Hija 1445

Mikakati 8 Muhimu ya Kuzuia Kiharusi cha Joto Wakati wa Hija

10:39 - June 10, 2024
Habari ID: 3478957
IQNA - Katika kilele cha msimu wa joto kali katika Ufalme wa Saudi Arabi, mamilioni ya Waislamu ulimwenguni kote wamekusanyika Makka kutekeleza ibada ya Hija. Mkusanyiko huu mkubwa unaibua wasiwasi kuhusu changamoto zinazoweza kujitokeza katika siku zijazo.

Hali ya hewa isiyotabirika ya eneo hilo inahatarisha afya na usalama wa mahujaji, huku wazee wakiwa hatarini zaidi. Kuongezeka kwa halijoto duniani kumesababisha ongezeko la marudio na ukubwa wa mawimbi ya joto katika eneo hilo kila mwaka.

Wakati wa Hija ya mwaka uliopita, Makka ilikumbwa na halijoto ya kuanzia nyuzi joto 43 hadi 45 Selsiasi. Joto hili kali lilikuwa na athari kubwa kwa afya ya mahujaji, haswa wazee, ambao hukabiliwa na maswala yanayohusiana na joto kama vile kiharusi cha joto na upungufu wa maji mwilini.

Ayman bin Salem Ghulam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kitaifa cha Hali ya Hewa cha Saudia, hivi karibuni alifahamisha mkutano wa waandishi wa habari huko Makka kwamba viwango vya juu vya joto vya maeneo matakatifu vinatarajiwa kufikia kati ya nyuzi 45 na 48 wakati wa saa za alasiri.

Inafaa kumbuka kuwa mahujaji wengi wazee wana hali za kiafya zilizokuwepo ambazo zinaweza kuzidishwa na joto, na kuwafanya kuwa rahisi zaidi kukumbwa shida za kiafya.

Kuna, hata hivyo, mikakati ambayo inaweza kusaidia kuzuia kiharusi cha joto.

Mavazi

Mahujaji wanashauriwa kuchagua nguo za rangi nyepesi, ikiwezekana nyeupe, za pamba katika safari yote ya Hija. Wanapaswa kuepuka kuvaa nguo nyeupe zenye mada za plastiki, kwani hupelekea joto kubakia mwilini.

Kuwa na maji mwilini

Kuhakikisha kuwa daima mwili una maji ya kutosha, hasa kwa kuzingatia hali ya hewa ya Makka, ambapo upotevu wa maji kupitia jasho unaweza kutokea bila kutambuliwa.

Kiasi cha maji kinachohitajika kinaweza kutofautiana kulingana na hali ya kimwili ya mtu, kiwango cha shughuli za kimwili, umri, na jinsia. Ufuatiliaji wa rangi ya mkojo hutumika kama kiashiria cha kiwango cha maji mwilini; mkojo usio na rangi unaashiria maji ya kutosha mwilini kutosha, wakati mkojo wa manjano unaashiria hitaji la kuongezeka kwa matumizi ya maji.

Kujilinda na jua

Inapendekezwa kwa wanaume na wanawake kutumia mafuta ya kujipaka yenye kujilinda na miale ya jua, isipokuwa kwa siku chache wakati kuna vikwazo vya kidini. Miwani ya jua inapaswa kuvaliwa na wote.

Wanaume wanashauriwa kuvaa kofia zinazoweza kuleta kivuli kwenye uso, ikiwezekana nyeupe, ili kufunika uso na nyuma ya shingo ili kuzuia kuchomwa na jua.

Wanawake wanaweza kufikiria kuvaa kofia ya rangi angavu na kutumia miavuli ili kuepuka kupigwa na joto na kuchomwa na jua.

Mpango wa Harakati

Kupunguza harakati za kidini katika Hija kama vile kuzunguka al Kaaba au kutufu wakati wa mchana kuna manufaa.

Kufanya shughuli hizi baada ya jua kutua kunaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kiharusi cha joto.

Epuka kutembea wakati wa jua kali

Mahujaji wanashauriwa kujaribu kuepuka kupigwa na jua kwa wingi, hasa kati ya saa 10 asubuhi hadi saa tisa alasiri.

Maeneo yenye kivuli

Kuongeza muda unaotumiwa katika mazingira ya baridi au yenye kiyoyozi hewa na kutafuta kivuli kunaweza kuwa na manufaa.

Miavuli

Kutumia miavuli yenye rangi nyepesi hutoa ulinzi wa ziada wa jua.

Pumzika

Usingizi wa kutosha na kupumzika ni muhimu, na ni busara kutekeleza ibada ya Hija kwa taratibu ili kuzuia uchovu.

Wakati huo huo, mamlaka ya Saudia imetangaza utekelezaji wa hatua za kupunguza hali ya joto inayoongezeka, kama vile kupanua maeneo yenye kivuli, kusambaza maji ya kunywa, na kuweka mifumo ya hali ya hewa kwenye maeneo matakatifu.

3488668

Kishikizo: hija makka
captcha