IQNA

Hija

Saudi Arabia kuwaadhibu wanaofika Hija bila kibali

16:26 - May 09, 2024
Habari ID: 3478797
IQNA - Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi Arabia imetangaza kanuni kali zaidi za Hija mwaka huu, inayolenga wale wanaoshiriki ibada ya Hija bila kibali na pia wale wanaowasaidia kukiuka sheria

Wakiukaji, ikiwa ni pamoja na wale wanaosafirisha watu ambao hawajaidhinishwa kwenda Hija, watakabiliwa na adhabu ikiwa ni pamoja na kifungo cha miezi sita jela na faini ya Riyal 50,000 za Saudi (takriban dola 13,333), kulingana na taarifa ya wizara mnamo Jumanne.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi Arabia iliongeza kuwa kuwepo katika maeneo maalum ya Hijja bila kibali halali ni kosa kubwa, linalowahusu wote, bila kujali iwapo wana idhini ya kuishi Saudia.

Wakaazi wanaokiuka sheria wanaweza kukabiliwa na kufukuzwa Saudia  na kupigwa marufuku kuingia tena kwa muda uliowekwa na sheria.

Wizara ilionya wahalifu ambao watapatikana kuwa wamewahi fanya kosa hilo watakabiliwa na adhabu kali zaidi, ikiwa ni pamoja na kifungo, faini, na uwezekano wa kunyang'anywa magari.

Kanuni hizo mpya zitatekelezwa kote Makka, Ukanda wa Kati unaozunguka, maeneo matakatifu, kituo cha treni cha Haramain huko Rusaifah, vituo vya ukaguzi vya usalama, vifaa vya kupanga na vituo vya usalama vya muda kuanzia tarehe 2 Juni 2024 hadi Juni 20, 2024.

Utekelezaji huu unafuatia agizo la hivi majuzi la mamlaka ya Saudi kuwataka watu wote kutoka nje kupata vibali kabla ya kuingia Makka. Kuanzia Mei 4, 2024, ni lazima wahamiaji wapate kibali kutoka kwa mamlaka husika kabla ya kuingia katika jiji hilo takatifu.

Hija katika mji mtakatifu wa Makka ambayo kila Mwislamu mwenye uwezo wa kimwili na uwezo wa kifedha anapaswa kutekeleza angalau mara moja katika maisha yake, na ni moja ya nguzo za Uislamu na ni mjumuiko mkubwa zaidi wa aina yake duniani.

Aidha ni dhihirisho la umoja wa Waislamu na kujisalimisha kwao kwa Mwenyezi Mungu. Hajj ya mwaka huu itafanyika kati ya Juni 2 na Juni 20.

3488259

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hija makka
captcha