IQNA

Maqarii wa Qur'ani duniani waomboleza vifo vya maqarii wa Iran Mina

11:35 - September 27, 2015
Habari ID: 3372181
Maqarii wa Qur'ani kutoka pembe mbali mbali duniani hasa Misri wanaendelea kuomboleza vifo vya maqarii wawili mashuhuri wa Iran waliokuwa wakitekeleza ibada ya Hija katika eneo la Mina karibu na mji mtakatifu wa Makkah.

Miongoni mwa mahujaji takribani 2,000  wakiwemo Wairani 136 waliothibitishwa kupoteza maisha katika maafa ya Mina Alhamisi iliyopita, walikuwemo maqarii wawili wa kimataifa wa Iran, Mohsen Hajihassani Kargar na Amin Bavi.
Maustadhi waandamizi wa Qur'ani Misri Ahmad Ahmad Noaina, na Muhammad Taha Abdul Wahab.
Katika ujumbe wake, Ustadh Noaina ameliitaja tukio la Mina kuwa maafa makubwa na kutuma salamu zake za rambi rambi kwa jamii ya Qur'ani nchini Iran na familia za maqarii hao wawili. Naye Ustadh Abdul Wahab ametuma salamu zake za rambi rambi kufuatia vifo vya maqarii hao  wawili.
Ustadhi wa Qur'ani kutoka Iran Adnan al Salehi na qarii wa kimatiafa Yahya al Sahaf pia wametuma salamu za rambi rambi kufuatia vifo vya Hajihassani Kargar and Bavi.../mh

3370927

captcha