Wanajeshi hao wa utawala wa Kizayuni Israel pia waliwashambulia Waislamu wa Palestina waliokuwa ndani ya msikiti huo kwa risasi na gesi ya kutoa machozi.
Wakati huo huo magenge ya walowezi wa Kiyahudi wenye misimamo ya kufurutu ada waliokuwa wakisaidiwa na wanajeshi wa Israel walishambulia eneo la Babul Silsila katika Msikiti wa al Aqsa kwa lengo la kuchochea Waislamu waliofanya mgomo ndani ya msikiti huo na kukabiliwa na majibu makali ya Wapalestina.
Eneo la Msikiti wa al Aqsa limekuwa uwanja wa mapigano makali baina ya wanajeshi wa Israel na Wapalestina tangu wiki mbili zilizopita kutokana na hujuma ya walowezi wa Kizayuni waliokwenda eneo hilo kwa kutumia visingizio mbalimbali. Makumi ya Wapalestina wamejeruhiwa katika hujuma hizo na wengine wengi wametiwa nguvuni na kupelekwa kusikojulikana na askari wa utawala bandia wa Israel.