IQNA

Chuo cha Sayansi za Qur’ani kuanzishwa Misri

13:58 - October 29, 2015
Habari ID: 3409344
Ujenzi wa Chuo cha Sayansi za Qur’ani cha Al Hussary umezinduliwa katika mkoa wa Minya nchini Misri.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA,  uzinduzi wa ujenzi huo umezinduliwa katika sherehe iliyohudhuriwa na Yasmin al-Hussary bintiye Sheikh Mahmoud Khalil al Hussary, qarii mashuhuri wa Qur’ani nchini Misri ambaye ameanzisha mradi huo. Wengine waliohudhuria uzinduzi huo ni Sheikh Umar Abdul Kafi mhubiri maarufu Misri na Mahmoud Abdul Hafiz, mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Al Azhar.
Chuo hicho kitakuwa tawi la Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al Azhar  na pia kinafungamana na Kituo cha Mani Mazar katika mji wa Bahnasa kaskazini mwa Minya.
Lengo la kuanzishwa chuo hicho ni kuwahudumia wanafunzi wa Qur’ani Tukufu katika eneo hilo la Misri.

3394869

Kishikizo: misri qurani chuo sayansi
captcha