Kwa mujibu wa gazeti la The Nation la Nigeria, hatua hiyo itarejesha hadhi ya jimbo la Yobe kama kitovu cha masomo ya Qur'ani. Katika zama za kale, Ufalme wa Borno uliojumuisha majimbo ya Yobe na Borno ulikuwa mashuhuri kwa masomo ya Qur'ani na sayansi za Kiislamu kote katika bara la Afrika.
Hivi sasa kwa msaada wa serikali ya jimbo, Chuo Kikuu cha Yobe kinapanga kurejesha hadhi ya masomo ya Qur'ani katika eneo hilo.
Chuo hicho kimeancisha Taasisi ya Utafiti wa Masomo ya Qur'ani ili kuhakikisha kuwa mfumo wa masomo ya Qur'ani yanaendeshwa kwa kuzingatia ustawi wa sayansi na teknolojia nchini Nigeria na kote katika ulimwengu wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa Naibu Kansela wa Chuo Kikuu cha Yobe Profesa Musa Alabe, kituo hicho pia kitakuwa na jukumu la kukabuliana na misimamo mikali ya kidini inayoenezwa na kundi la magaidi wakufurishaji wa kundi la Boko Haram.