IQNA

Hizbullah Kulipiza Kisasi Baada ya Israel Kumuua Qantar

10:46 - December 22, 2015
Habari ID: 3468139
Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imesema itatoa jibu kali kwa mauaji ya kamanda wake mwandamizi Samir Qantar, yaliyofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel.

Akihutubia umati mkubwa kwa njia ya televisheni, uliohudhuria mazishi ya Qantari mjini Beirut hapo jana, Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah amesema harakati hiyo ina haki ya kujibu mapigo ya mauaji hayo. Sayyid Hassan Nasrullah amesema hawana shaka kuwa mauaji hayo yalitekelezwa na makombora ya ndege za utawala haramu wa Israel.
Mapema jana maelfu ya watu walihudhuria mazishi ya Samir Qantari mjini Beirut. Jamhuri yua Kiislamu ya Iran imelaani ukatili huo na kusema kuwa, mauaji hayo ni mfano mwingine wa ugaidi wa kiserikali wa utawala ghasibu wa Israel.
Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel usiku wa kuamkia Jumapili zilishambulia nyumba moja katika mji wa Jaramana huko kusini mwa Damascus, mji mkuu wa Syria na kumuua shahidi Samir Qantar ambaye alikuwa miongoni mwa makamanda waandamizi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

3468010

captcha