Waziri Mkuu wa jimbo la Keda Mukhriz bin Mahathir amesema kundi kigaidi la ISIS linatumia vibaya aya za Qur'ani na hivyo kuwahadaa baadhi ya Waislamu kufuata kundi hilo la wakufurishaji.
"Tuna wasiwasi kuhusu ISIS kuwashawishi Waislamu, hasa vijana, ambao wana ufahamu duni kuhusu dini," amesema Mahathir.
"Nalitazama suala hili kwa uzito mkubwa kwa sababu sitaki ushawishi wa ISIS katika nchi yetu. Lazima tuchukue hatua za haraka na nimeitaka afisi ya Mufti ikabiliane na tishio la ISIS."
Mukhriz bin Mahathir ametoa wito kwa wanakijiji katika jimbo lake kuchukua hatua za haraka iwapo watagundua harakati zozote za kundi la ISIS nchini humo.
Kundi la magaidi wakufurishaji wa ISIS au Daesh wanafuata itikadi potovu za Kiwahhabi na hivi sasa wameteka maeneo kadhaa ya Syria, Iraq na Libya ambako wanatekeleza jina na ukatili mkubwa.