Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, warsha hiyo ya siku mbili imeandaliwa na na Taasisi ya Idrak na itafanyika katika eneo la Al Khuwair mjini Muscat.
Imearifiwa kuwa washiriki wa warsha hiyo wataangazia namna ya kushukuru kwa kuzingatia yaliyomo katika Suurat An Nahl.
Kikao hicho cha Tadabbur au mazingatio katika Qur'an Tukufu kitaongozwa na Ustadh Salah Al Liyafy ambaye pia ni mwalimu wa Aklhalqi.
Warsha hiyo itaangazia maudhui kama vile "ufahamu wa kushukuru katika Qur'ani Tukufu", "ibada ya kushukuru katika maisha ya kila siku" na "kutekeleza mafundisho ya Suurat An Nahl katika maisha ya kawaida."