Kwa
mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yatawashirikisha watu kutoka
makundi yote ya umri hasa vijana na mabarobaro wapatao 300 ambapo kutakuwa na
vitengo tafauti vya wanawake na wanaume.
Halikadhalika mashindano hayo yatawashirikisha raia wa kigeni waishio Oman na wanafunzi vya vyuo vikuu na wake nyumbani.
Mashindano hayo yatakuwa na kategoria za kuhifadhi Juzuu moja, Juzuu 15, Juzuu 20 na Sura al Kahf kwa kuzingatia misingi ya tajweed katika kusoma Qur’ani Tukufu.
Washindi watapata zawadi za fedha taslimu na cheti cha kushiriki.