IQNA

Mmarekani wa kwanza kushiriki Olympiki akiwa amevaa Hijabu

10:32 - February 04, 2016
Habari ID: 3470114
Ibtihaj Mohammad anatazamiwa kuwa mwanamichezo wa kwanza Mmarekani kushiriki katika michezo ya Olympiki akiwa amevalia Hijabu.








Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mwislamu huyu mwenye umri wa miaka 30 ambaye daima huvaa vazi la staha la Hijabu akiwa mashindanoni na anatazamiwa kushiriki katika michezo ya Olympiki mwaka 2016 nchini Brazil akiwa amevalia Hijabu katika mchezo wa vitara (fencing).

Alipata nishani ya shaba katika Kombe la Dunia la Wanawake la Mchezo wa Vitara Jumamosi iliyopita na hivyo kufuzu kuingia katika timu ya ni mchezo wa vitara ya Marekani katika Michezo ya Olympiki ya Rio, Brazil.

"Wakati watu wengi wanapo tasawari mcheza vitara katika Olympiki, aghalabu huwa hawatazamii kuona mtu kama mimi. Kwa bahati nzuri, mimi si aghalabu ya watu," anafafanua. "Daima nimekuwa na imani kuwa, nikifanya kazi kwa bidii na nidhamu, siku moja nitajiunga na timu ya Marekani na kuweka historia katika Olympiki."

Anasema anataka kushiriki katika Olympiki ili kuthibitisha kuwa, hakuna chochote kinachoweza kumzuia yeyote kufkia malengo yake, si rangi, dini au jinsia. "Nataka kuwa mfano hai kuwa, kila kitu kinawezekana kwa ustahamilivu," anasema Ibtihaj Muhammad.

Mwenyeji huyo wa New Jersey anasema akiwa na umri wa miaka 13, alianza mchezo wa vitara.

3472785

captcha