IQNA

Russia yawakamata magaidi wa ISIS, yazuia hujuma za kigaidi

21:09 - February 08, 2016
Habari ID: 3470122
Vikosi vya usalama Russia vimewakamata magaidi saba wa kundi la ISIS (Daesh) ambao walikuwa wanapanga kutekeleza hujuma za kigaidi katika miji kadhaa kote Russia.

Kikosi cha Polisi wa Upelelezi Russia, FSB, imetangaza kuwakamata magaidi hao wakufurishaji wakiwemo raia wa Russia na pia wengine wenye utaifa wa nchi za Kati mwa Asia. Kwa mujibu wa shirika la habari la Interfax, magaidi hao wamekamatwa katika mji wa Yekaterinburg eneo la Urals. FSB imesema magaidi hayo walikuwa wanapanga kutekeleza hujuma za kigaidi katika mji mkuu Moscow na mji wa St Petersburg na pia katika eneo la Sverdlovsk huko Urals.

Taasisi hiyo ya usalama Russia imeongeza kuwa magaidi hao walikuwa wakiongozwa na gaidi wa ISIS aliyeingia nchini humo akitokea Uturuki.

Siku chache zilizopita, Andrey Przhezdomsky, msemaji wa Kamati ya Kitaifa ya Russia ya kupambana na ugaidi alisema mitandao ya kigaidi inayofungamana na magaidi wa ISIS walikuwa wakipanga kutekeleza hujuma Russia na bara Ulaya.

Russia inasema mwaka 2015 iliwazuia raia wake zaidi ya 100 waliokuwa wanapanga kuondoka nchini humo kujiunga na magaidi wa ISIS. Wakuu wa usalama Russia wanakadiria kuwa kuna magaidi kati ya 5000 hadi 7000 kutoka nchi zilizokuwa katika shirikisho la Sovieti ambao wamejiunga na magaidi wa ISIS Syria na Iraq.

Tokea Septemba 30 mwaka jana, Russia imekuwa ikitekeleza hujuma dhidi ya

Tokea Septemba 30 mwaka jana, Russia imekuwa ikitekeleza hujuma dhidi ya ISIS na magaidi wengine nchini Syria kufuatia ombi la serikali ya Damascus.

3474064

captcha