IQNA

Nakala 130,000 za Qur'ani kusambazwa Mauritania

12:02 - February 20, 2016
Habari ID: 3470152
Nakala 130,000 za Qur'ani zinasambazwa nchini Mauritania kote katika nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Taasisi ya Kutoa Misaada ya Taawon imezindua mpango huo wa kusambaza nakala za Qur'ani katika madrassah za Qur'ani na taasisi za kielimu kote katika nchi hiyo ya kaskazini magharibi mwa Afrika.

Sheikh Omar al Fath, mkurugenzi wa taasisi hiyo amesema kamati maalumu ya wanazuoni imeundwa kwa lengo la kutembelea miji na vijiji vya nchi hiyo ili kubaini mahitajio ya madrassah na vyuo vya Qur'ani.

Amesema vituo 45 vitapokea nakala hizo za Qur'ani kote Mauritania na kwamba mradi hiyo umefadhiliwa na raia mmoja wa Bahrain aliyetambuliwa kama Abdul Ghaffar Abdul Rahim al-Kahuji.

Mauritani ni nchi ya Kiislamua yenye idadi ya watu milioni nne ambao karibu wote ni Waislamu.

3476692

captcha