IQNA

Al Arabiya yamfuta kazi aliyerusha filamu kumhusu Nasrallah

17:26 - February 23, 2016
Habari ID: 3470157
Mkurugenzi wa Kanali ya Televisheni ya Kiarabu ya Al Arabiya amefutwa kazi kwa kutangaza filamu ya kweli ambayo ilionekana kumuunga mkono kiongozi wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrallah.

Shirika la matangazo ya satalaiti la Saudi Arabia lijulikanalo kama Middle East Broadcasting Centre Group MBC, ambalo linamiliki Al Arabiya, limetangaza kumfuta kazi mwandishi habari mwandamizi Turki bin Abdullah Aldakhil.

Uamuzi huo umechukuliwa siku chache tu baada ya Al Arabiya kurusha hewani filamu ya matukio ya kweli au documentary yenye anwani ya ‘Kisa cha Hassan’ ambayo iliangazia maisha ya Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah.

Aldakhil mwenye umri wa miaka 42 alianza kazi ya uandishi wa habari mwaka 1989 katika magazeti kadhaa kama vile al-Riyadh, Okaz, Asharq al-Awsat, al-Majalla na pia al-Hayat. Aljiunga na MBC na kisha Al Arabiya mwaka 2003 na kupanda cheo hadi kuwa mkurugenzi wa stesheni hiyo.

Al Arabiya yamfuta kazi aliyerusha filamu kumhusu Nasrallah

Hii si mara ya kwanza kwa Saudi Arabia kuwaadhibu waandishi huru wa vyombo vya habari.

Mwezi Disemba utawala wa Saudia ulisitisha matangazo ya kanali ya televisheni ya Hizbullah ya Al Manar katika satalaiti ya Arabsat. Aidha mwezi Januari Saudia ilishurutisha shirika la Arabsat kusitisha matangazo ya televisheni nyingine ya Lebanon, Al Mayadeen. Shirika la Arabsat lina makao makuu yake mjini Riyadh na Saudia inamiliki asilimia 36 ya hisa katika shirika hilo la kurusha matangazo ya satalaiti.

3477822

captcha