IQNA

7:17 - March 10, 2016
News ID: 3470189
Watu 16 wenye ulemavu wa macho wameshiriki katika mashindano ya kitaifa ya Qur’ani Iran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yamefanyika Jumatano ambapo kulikuwa na washiriki 16. Watakaofuzu katika mashindano hayo ya kuhifadhi Qur’ani wataiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya wenye ulemavu wa macho.

Majaji katika mashindano hayo walikuwa na maustadh bingwa wa Qur’ani, ambao ni Ali Akbar Hanifi, Rahim Khaki, Saeed Rahmani, Amir Aghayi and Habib Mahkam.

Mashindano ya kwanza ya kimataifa ya Qur’ani ya wenye ulemavu wa macho yatafanyika nchini Iran baadaye mwaka huu pembizoni mwa Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu.

Zaidi ya nchi 30 tayari zimeshatangaza kutumwa wawakilishi wao katika mashindano hayo ya wenye ulemavu wa machi.

Mashindano ya kwanza ya kimataifa ya Qur’ani ya wenye ulemavu mwaka huu yatakuwa na kategoria ya kuhifadhi tu lakini kategoria nyingine zitaongezwa katika mashindano ya mustakabali.

3482051

Tags: IQNA ، ، ، ،
Name:
Email:
* Comment: