IQNA

Rais Rouhani ampongeza Kiongozi Muadhamu kwa munasaba wa mwaka mpya wa Hijria Shamsia

11:47 - March 22, 2016
Habari ID: 3470209
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amempa mkono wa kheri na fanaka Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa kuwadia mwaka mpya wa 1395 Hijria Shamsia.

Katika mazungumzo hayo ya simu waliyofanya hii leo kufuatia kuanza mwaka Mpya wa Hijria Shamsia, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mkono wa kheri kwa kuwadia mwaka mpya wa 1395 na kumuombea afya njema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusisitiza pia kuwa mwaka mpya wa 1395 Hijria Shamsia utakuwa mwaka wa matarajio na juhudi za pande zote kwa ajili ya kuijenga Iran bora kwa watu wa nchi hii.

Rais Rouhani ameongeza kuwa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatumia uwezo wake wote katika kutekeleza katiba, mipango ya kistratejia ya Iran na miongozo ya Kiongozi Muadhamu.

Katika mazungumzo hayo ya simu naye Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amempongeza Rais Rouhani kwa kuwadia mwaka mpya wa 1395 Hijria Shamsia na familia kubwa ya taifa la Iran na kuiombea pia serikali mafanikio zaidi ili kuweza kuiahudumia Iran na wananchi.

3484317

captcha