IQNA

Nchi za Kiislamu kujadili kadhia ya Palestina nchini Uturuki

18:28 - April 11, 2016
Habari ID: 3470241
Nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC Jumapili zimeanza mkutano wao wa kila mwaka Istanbul, Uturuki huku kadhia ya Palestina, migogoro katika nchi wanachama na ugaidi zikiwa mada zitakazopewa kipaumbele.

Mkutano huo wa nchi 57 za OIC unakuja katika kipindi ambacho nchi nyingi za Waislamu zinakumbwa na migogoro ambapo magaidi wanaopata himaya ya kigeni wameitumbukiza Syria vitani tokea mwaka 2011 na Yemen nayo ikikabiliwan na hujuma ya kinyama ya Saudi Arabia na waitifaki wake kwa zaidi ya mwaka moja.

Mkutano huo wa OIC ulianza Jumapili kwa mkutano wa wataalamu huku mawaziri wa mambo ya nje wan chi wanachama wakitazamiwa kukutana Jumanne na Jumatano. Marais zaidi ya 20 wanatazamiwa kuhudhuria mkutano wa kilele wa OIC siku za Alhamisi na Ijumaa.

Itakumbukwa kuwa yapata miaka 47 iliyopita iliasisiwa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) iliundwa. Jumuiya hiyo ni ya pili kwa ukubwa baada ya Umoja wa Mataifa kwa kuwa na nchi wanachama 57 katika mabara zaidi ya manne. Jumuiya hiyo inahesabiwa kuwa sauti ya ulimwengu wa Kiislamu yenye jukumu la kulinda maslahi ya Waislamu, kueneza moyo wa amani na kuratibu masuala ya Waislamu. Jumuiya hiyo iliundwa katika mkutano wa Kihistoria uliofanyika Rabat nchini Morocco tarehe 25 Septemba mwaka 1969 kama jibu la hatua ya Wazayuni wa Israel ya kuchoma moto Msikiti wa al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem)

OIC imekuwa ikikosolewa na Waislamu kote duniani kwa kushindwa kuchukua hatua za kivitendo kukabiliana na utawala ghasibu wa Israel ambao unaendele akukalia kwa mabavu ardhi za Palestina hasa Quds Tukufu.



3487706
captcha