IQNA

Qarii wa Al-Masjid an-Nabawi (SAW) aaga dunia

17:39 - April 16, 2016
1
Habari ID: 3470249
Sheikh Mohammad Ayub ibn Yusuf, msomaji na qarii wa Qur'ani Tukufu katika Al-Masjid an-Nabawi mjini Madina ameaga dunia leo Aprili 16 akiwa na umri wa miaka 65.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mwanae wa kiume wa Sheikh Mohammad Ayub ametangaza habari za kuaga dunia baba yake kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kwa kuandika hivi: " Sheikh Ayub atazikwa baada ya sala ya Alasiri katika makaburi ya Baqi."

Mohammad Ayub alizaliwa mwaka 1372 Hijria Qamaria katika mji wa Madina. Akiwa na umri wa miaka 12 alihifadhi Qur'ani kikamilifu akiwa anapata mafunzo ya msingi kutoka kwa Sheikh Zaki Daghistani, na Sheikh Khalil. Aidha Sheikh Mohammad alisoma tafsiri ya Qur'ani kutoka kwa maustadhi bingwa kama vile Sheikh Muhammad Sayyid Tantawi, Sheikh Abdulaziz Muhammad Othman, Sheikh Akram Dhiya Al-Amri, Sheikh Muhammad Al-Amin Al-Shiqiti and Sheikh Abdulmuhsin Al-Abbad.

Hayati Sheikh Ayub alikuwa na harakati nyingi za Qur'ani kama vile qiraa yake ya Qur'ani kikamilifu kurekodiwa na kurushwa hewani katika Radio ya Qur'ani Saudia. Aidha alikuwa akiswalisha Salatul Tarawih katika Al-Masjid an-Nabawi wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kila mwaka.

3489060


Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
abdillahkikuru
0
0
Allah amfungulie milango ya Janna wallah hii ndio khusnil khaatima
captcha