IQNA

Iran na Uganda kushirikiana katika masuala ya Qur'ani

13:38 - April 18, 2016
Habari ID: 3470252
Mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Iran mjini Kampala amekutana na Mufti Mkuu wa Uganda na kujadilia njia za kushirikiana nchi mbili katika harakati za Qur'ani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Ali Bakhtiari, Mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Iran mjini Kampala alimtembelea Mufti Mkuu wa Uganda Sheikh Siliman Kasule Ndirangwa na kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala kadhaa.

Kati ya waliyoyajadili ni ushirikiano katika uga wa harakati za Qur'ani, kutoa mafunzo kwa familia na vijana na kuandaa mashindano ya Qur'ani katika vyuo vikuu.

Katika kikao hicho Sheikh Siliman Kasule Ndirangwa ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ushirkiano wake wa muda mrefu na Ofisi ya Mufti wa Uganda.

Aidha amepongeza jitihada za Iran kuwaunga mkono Waislamu na nchi za Kiislamu duniani na kusema jambo hilo litachangia kupatikana umoja wa Waislamu. Ameogeza kuwa: "Sisi tuko tayari kutoa ushirikiano wowote ambaon utaimarisha Waislamu na kuleta umoja wa Kiislamu."

Kwa upande wake mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Iran mjini Kampala amempongeza Sheikh Siliman Kasule Ndirangwa kwa kuteuliwa kuwa Mufti Mkuu wa Uganda. Aidha ameashiria hali ya hivi sasa ya Ulimwengu wa Kiislamu na dharura ya kupambana na misimamo mikali ya kidini. Amesema maadui wanatekelez anjama nyuma ya pazia kwa lengo la kuchochea mifarakano baina ya Waislamu.

3489630

Kishikizo: iqna uganda waislamu
captcha