Ndugu hao wawili, wenye umri wa miaka 14 na 15 , wameibua mjadala mkali Usiwisi kwa hatua yao hiyo ambayo inaenda sambamba na mafundisho ya Kiislamu ya wanawake na wanaume ajinabi kutopeana mikono.
Awali wanafunzi hao wa kiume Waislamu wa Manispaa ya Therwil katika jimbo la Basel nchini Uswisi walikuwa wamepata idhini ya kutowapa mikono walimu wao wa kike kufuatia uamuzi uliotolewa Mamlaka za Elimu katika eneo hilo.
Maafisa wa elimu wa eneo la Therwil walifikia uamuzi huo ambao ulizusha mjadala na makelele nchini Uswisi baada ya wanafunzi wawili wa kiume Waislamu kualalmika kwamba mila na desturi za Uswisi za kupeana mikono na mwalimu zinakinzana na imani yao ya kidini endapo mwalimu huyo atakuwa ni wa kike. Wanafunzi hao walibainisha katika malalamiko yao kuwa Uislamu hauruhusu mtu kugusana kimwili na mwenzake wa jinsia tofauti isipokuwa watu ambao ni maharimu zake katika familia.
Hata hivyo uamuzi huo ulioptishwa na Mamlaka za Elimu katika eneo hilo umezusha makelele nchini Uswisi. Felix Mueri mkuu wa Kamati ya Bunge ya Sayansi, Elimu na Utamaduni amesisitiza kuwa kupeana mikono ni sehemu ya utamaduni wa nchi hiyo.
Baba ya vijana hao ambaye ni imamu wa msikiti mmoja mjini Basel na ambaye ni
raia wa Syria aliwasilia Uswisi mwaka 2001 na kupata hifadhi ya kisiasa. Kuna
Waislamu 350,000 katika jamii ya watu milioni nane nchini Uswisi.