Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kituo hichi kitakuwa na uwezo wa kutoa mafunzo kwa wanafunzi 3500 wanaohifadhi Qur'ani na 450 wanaojifunza sayansi za Qur'ani na dini.
Kwa mujibu wa Sheikh Abbas Motaqedi, Mkuu wa tawi la Senegal la Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW, kituo hicho cha kufunza Qur'ani au Darul Qur'an kilizinduliwa rasmi mwaka 1939 na Sheikh Ahmed al-Saqir kwa lengo la kufunza Qur'ani na sayansi za Qur'ani.
Amesema kuwa kituo hicho kimekuwa kikiimarika tokea mwaka 1971 kwa uungaji mkono wa wafadhili wa eneo hilo.
Mapemza mwezi huu Motaqedi na Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Senegal Seyyed Hassan Esmati alitembelea kituo cha Darul Qur'an katika eneo la Louga, kilomita 200 kaskazini mwa mji mkuu wa Senegal ,Dakar. Akiwa hapo alikutana na mkurugenzi wa kituo hicho Sheikh Mukhtar Nar Luh ambapo walijadili njia za ushirikiano wa pamoja na ustawishaji wa uhusiano katika nyuga za Qur'ani na utamaduni.
Asilimia 92 ya watu wote miluioni 14.5 wa Senegal ni Waislamu.