Bingwa huyo wa zamani wa mchezo wa Masumbwi Dunia kwa uzito wa juu (World Heavyweight Champion) ameaga dunia katika hospitali moja mjini
Phoenix jimbo la Arizona, alikolazwa tangu Alkhamisi iliyopita kutokana
na matatizo ya kupumua.
Imearifiwa kuwa, matatizo hayo ya kupumua
yalitokana na ugonjwa wa kutetemeka alioupata tangu mwaka 1984. Msemaji
wa familia ya Muhammad Ali amewashukuru wote waliosimama na nyota huyo
wa ndondi alipokuwa anaugua hadi wakati wa kifo chake na kusisitiza kuwa
kwa sasa familia hiyo inahitaji faragha. Taarifa ya familia ya
mwanamasumbwi huyo imesema bingwa huyo mara 3 wa mashindano ya kimataifa
ya Olimpiki atazikwa nyumbani kwake mjini Louisville, eneo la Kentucky.

Itakumbukwa kuwa, bingwa huyo wa ndondi aliyejiunga na mchezo huo
akiwa na umri wa miaka 12, alifahamika kama Cassius Clay, lakini
akabadilisha jina na kuitwa Muhammad Ali baada ya kujiunga na dini
tukufu ya Kiislamu mwaka 1964.
3503744