IQNA

Bustani mjini Detroit, Marekani kupewa jina la Muhammad Ali

17:28 - February 14, 2022
Habari ID: 3474929
TEHRAN (IQNA)- Bustani ya Belton-Mark Twain mjini Detroit, jimbo la Michigan la Marekani, ina jukumu muhimu katika kusaidia familia za karibu kupata bustani nzuri ya kupumzika.

Hitajio hilo la eneo la mapumziko nje ya nyumba ni  ni moja ya motisha kubwa kwa Kituo cha Kiislamu cha Detroit katika kufanyia ukarabati  Bustani ya Belton-Mark Twain .

"Sababu ya kuiita bustani hiyo Muhammad Ali si dini tu bali ni kwamba alikuwa mfano wa kuigwa wa Mwislamu, na pia allikuwa maarufu kutokana na uwezo wake wa kujenga," amesema afisa mtendaji wa  Kituo cha Kiislamu cha Detroit Rawan Shihab.

Shihab anasema mpango wa ukarabati wa bustani hiyo utagharimu $350,000 na unalenga kufanya bustani kuwa mahali salama, pa kupendeza, na mahali penye mwelekeo wa familia kwa wote. Itakuwa na eneo la kuchezea, eneo la pikniki, uwanja wa soka, uwanja wa mpira wa vikapu na njia ya kukimbia au ya kutembea.

Meneja wa Wilaya ya 7 ya Detroit Mona Ali anasema jiji hilo linaunga mkono juhudi za kituo hicho za kufufua bustani hiyo, lakini mchakato wa kubadilisha jina utakuwa kwa baraza la jiji mara tu mahitaji ya ombi la jumla ya sahihi 500 yatakapotimizwa.

Mwaka jana Kituo cha Kiislamu cha Detroit ilitoa karibu milo milioni 10 kwa jamii.

Michango yao ya mwaka mzima pia ilisaidia maelfu ya familia kote Michigan.

Shihab anasema kituo hicho ni mojawapo ya mashirika ya kutoa misaada katika jimbo lote na husaidia mtu yeyote anayehitaji.

"Hasa wale wanaokuja wapya, kama wakimbizi na sio wakimbizi, na jamii kwa ujumla sio tu jamii ya Waislamu, tumekuwa tukijaribu kufanya kila tuwezalo kwa ubora iwe ni katika afya ya akili au msaada wa chakula," Shihab alisema.

Muhammad Ali alikuwa Mwislamu Mmarekani nnguli wa masumbwi duniani  na alifariki Juni 3 2016  akiwa na umri wa miaka 74, baada ya kuugua ugonjwa wa kutetemeka kwa muda mrefu.

Bingwa huyo wa ndondi mwenye asili ya Afrika, alikuwa akijulikana kama Cassius Clay kabla ya kusilimu na kuitwa Muhammad Ali katika miaka ya 1960.

Muhammad Ali aliongoza harakati za kutetea usawa wa watu wa rangi zote bila ya ubaguzi.

3477810

captcha