Katika mahojiano na IQNA, Aizollah Mortazavi afisa mwandamizi wa Taasisi ya Darul Qur’an Karim ya Iran amesema nakala hizo za Qur’ani zimechapishwa kwa idhini ya shirika hilo.
Amesema katika kipindi sawa na hicho mwaka jana, kulichapishwa nakala 789,000 za Qur’ani Tukufu nchini jambo ambalo linaonyesha kupungua uchapishaji mwaka huu.
Taasisi ya Darul Qur’an Karim inahusika na kuidhinisha, kuratibu na kusimamisha uchapishaji wa Qur’ani katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kila mwaka maelefu ya nakala za Qur’ani huchapishwa nchini Iran na kusambazwa nchini na maeneo mengine duniani.