Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kikao hicho cha Qur’ani kimeandaliwa na Taasisi ya Darul Qur’ani ya Idara ya Usimamizi wa Haram ya Imam Hussein AS.
Idadi kubwa ya wanajeshi, maafisa wa usalama na wapiganaji wa kundi la kujitolea la wananchi lijulikanalo kama Hashd al-Shaabi, walishiriki katika kikao hicho cha kusoma Qur’ani Tukufu.
Maeneo ya Kaskazini na Magharibi mwa Iraq yamekuwa yakishuhudia mapigano na ukatili mbaya sana tokea magaidi wa ISIS wakalie kwa mabavu maeneo hayo kuanzia Juni mwaka 2014.
Katika miezi ya hivi karibuni wanajeshi wa Iraq wakishirikiana na wapiganaji wa kujitokea wamefanikiwa kukomboa maeneo mengi yaliyokuwa yakikaliwa kwa mabavu na ISIS.
Mapema wiki hii, Waziri wa Ulinzi wa Iraq alitangaza kuwa, wapiganaji wa kundi la kigaidi la ISIS wanaendelea kuzidiwa nguvu na vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo na wameendelea kuhama ngome zao na kukimbilia katika maeneo mengine.
Khaledal-Obaidi ametangaza kuwa, vikosi vya Iraq vimeendelea kupata mafanikio katika operesheni zake za kuwatimua katika ardhi ya nchi hiyo wapiganaji wa kundi la kigaidi la ISIS.