IQNA

Vyombo vya habari vyapuuza Waislamu Somalia wanaouawa na magaidi

10:29 - August 11, 2016
Habari ID: 3470515
Mwandishi mwenye asili ya Somalia amebaini kuwa vyombo vya habari vya Magharibi hupuuza na kutozingaita habari kuhusu Waislamu wanaouawa katika vitendo vya kigaidi hasa nchini Somalia.

Katika Makala aliyoiandika katika gazeti la Washington Post, Abdi Nor Iftin anatoa mfano na kusema tarehe 26 mwezi uliopita wa Julai, wakati magaidi walipomuua kasisi nchini Ufaransa, tukio hilo lilipewa umuhimu katika kurasa zote za mbele za magazeti ya nchi za magharibi. Lakini siku hiyo hiyo, wakati magaidi walipowaua zaidi ya watu 12 katika mji mkuu wa Somalia, tukio hilo halikupewa umuhimu na vyombo vya habari. Amesema tukio hilo lilipuuza hata baada ya kubainika kuwa mmoja wa magaidi alikuwa ni mbunge wa zamani wa Somalia.

Abdi Nor Iftin anasema kwa muda mrefgu alikuwa akihudumia mashirka ya kimataifa ya habari huko Mogadishu na mjini Nairobi, Kenya na anafahamu sera za vyombo vya habari vya Magharibi kuhusu habari kama hizo. Anasedma ugaidi umepelekea kuibuka chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi katika hali ambayo Waislamu duniani ndio waathirika wakuu wa ugaidi.

3521732

captcha