IQNA

Malalamiko baada ya Waislamu kuvunjiwa heshima Afrika Kusini

17:29 - September 16, 2016
Habari ID: 3470566
Wakaazii wa mji wa Tshwane nchini Afrika Kusini wamebainisha hasira zao baada ya kupatikana maandishi ukutani yenye kuwavunjia heshima Waislamu.

Katika maandishi hayo yaliyokuwa katika ukuta,mbali na kuwatusi Waislamu pia kulikuwa na kauli za kuwataka Waislamu waondoke eneo hilo. Halikadhalika kulikuwa na alama ya msalaba chini ya maandishi hayo dhidi ya Waislamu katika mtaa wa Eersterus mjini Tshwane katika mkoa wa  Gauteng kaskazini mwa Afrika Kusini

Diwani wa eneo hilo Benjamin Lawrence amesema vitendo kama hivyo vinashuhuydiw akwa mara ya kwanza katika eneo hilo na kuongoeza kuwa ni kinyume cha msingi wa mji huo ambao ni umoja wa wakaazi wake wote.

Aidha amesema vitendo kama hivyo havitaruhusiwa kuendelea na kuongeza kuwa, "Hatuwezi ruhusu vitendo kama hivi. Sisi ni jamii moja." Kiongozi huyo amesema wakaazi wa eneo hilo wanafuata dini za Kiislamu na Kikristo na kwa muda mrefu wameishi kwa maelewano.

Katika kubainisha upinzani wao kwa vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu, wakaazi Wakristo wa eneo hilo la Tshwane Afrika kusini wamefuta maandishi hayo yaliyojaa chuki. Viongozi wa eneo hilo wameafiki kuitisha kikao kujadili njia za kuzuia chuki dhidi ya Waislamu.

Msemaji wa Polisi eneo hilo Sam Shibambo amesema uchunguzi unafanyika.

Waislamu nchini Afrika Kusini wanakadiriwa kuwa ni asilimia karibu 3 ya wakaazi wote miliono 53 nchini humo. Uislamu unahesbiwa kati ya dini zinazokuwa kwa kasi zaidi nchini humo kutokana na idadi kubwa ya Waafrika wazalendo wanaosilimu kila siku.

3530489/


captcha