IQNA

Waislamu Afrika Kusini

Msikiti wa Afrika Kusini waadhimisha maka 170 kwa kikao cha Qur'ani

19:43 - October 30, 2024
Habari ID: 3479671
IQNA - Msikiti wa Barabara Kuu ya Claremont (CMRM) nchini Afrika Kusini umeadhimisha mwaka wa 170 tokea ujengwe. Maadhimisho hayo yamejumuisha kwa mkusanyiko wa Khatm al-Quran (kusoma Qur'ani Tukufu tokea mwanzo hadi mwisho) na kuenziwa wale wote ambao wamechangia katika historia ya msikiti huo.

Msikiti wa Afrika Kusini waadhimisha maka 170 kwa kikao cha Qur'ani
IQNA - Msikiti wa Barabara Kuu ya Claremont (CMRM) nchini Afrika Kusini umeadhimisha mwaka wa 170 tokea ujengwe. Maadhimisho hayo yamejumuisha kwa mkusanyiko wa Khatm al-Quran (kusoma Qur'ani Tukufu tokea mwanzo hadi mwisho) na kuenziwa wale wote ambao wamechangia katika historia ya msikiti huo.
Msikiti wa CMRM ulianzishwa mwaka wa 1854, na umesalia kuwa nguzo ya mwongozo wa kiroho, mshikamano wa dini mbalimbali, na haki ya kijamii kwenye Barabara Kuu ya Cape Town.
Katika kikao hicho cha maadhimisho kulikuwa na dhikr iliyoongozwa na Al-Ameen Dhikr Jama’ah, ikifuatiwa na qiraa ya Qur'ani nzim na hotuba zinazoakisi historia na ushawishi wa msikiti huo.
Abdud-Daiyaan Petersen, mtafiti wa nyaraka, alihutubu kuhusu  historia ya awali ya eneo la Claremont/Newlands, akieleza kuwa Kampuni ya Uholanzi ya India Mashariki (VOC) ilianzisha mashamba katika eneo hilo na kwamba Waislamu wa awali walifika hapa kama wakimbizi wa kisiasa kutoka Indonesia.
"Hatua ya Waislamu kuja kufanya kazi aktika mashamba kulileta Uislamu katika sehemu hii ya Cape Town," Petersen alielezea, akisisitiza kuwa eneo hilo lina turathi ya  Kiislamu iliyokita mizizi.
Simulizi za kihistoria ziliendelea kwa Profesa Aslam Fataar kutoka Chuo Kikuu cha Stellenbosch kumtunuku zawadi Imam Gassan Solomons, kiongozi wa zamani wa Msikiti wa CMRM ambaye alitumia minbar ya msikiti huo kupinga ubaguzi wa rangi kwa mtazamo wa Kiislamu. "Imam Gassan amekuwa mkuu wa chemchemi, kwa kutangaza msimamo imara wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu akiwa katika minbar ya CMRM," Fataar alisema.

3490479

Kishikizo: waislamu afrika kusini
captcha