IQNA

Ayatullah Muhsin Araki

Marekani na Israel zinaibua mifarakano baina ya Waislamu

18:06 - February 13, 2017
Habari ID: 3470848
IQNA-Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu amesema: "Maadui wa Uislamu hasa Marekani na Utawala wa Kizayuni wa Israel wanatumia uwezo wao wote kuibua mifarakano katika Ulimwengu wa Kiislamu."

Ayatullah Muhsin Araki, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kukuribisha Madhehebu ya Kiislamu yenye makao yake Tehran ameyasema hayo katika mkutano aliofanya na maulamaa wa Kishia na Kisunni huko Hyderabad nchini India. Ameongeza kuwa, kama ambayo katika Qur'ani Tukufu na Sunna ya Mtume SAW tunavyosoma, ni wajibu wa jamii ya Kiislamu kufanya jitihada zaidi kuleta umoja miongoni mwa Waislamu wote na kuzuia adui kujipenyeza kiutamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Ayatullah Araki ameongeza kuwa, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu chini ya uongozi wa Imam Khomeini MA na hivi chini ya uongozi wenye busara wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kumekuwa na mabadiliko muhimu katika Ulimwengu wa Kiislamu na hivi sasa Uislamu halisi unaenea.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu amesema: "Jamii wa Kiislamu India na Maulamaa wa Kisuni na Kishia wanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuimarisha umoja na mshikamano wa Umma wa Kiislamu."

Ayatullah Araki aidha Jumapili usiku alishiriki katika kongamano la , "Umoja wa Umma katika Sira ya Bibi Fatima Zahra SA" mjini Heydarabad.

Akizungumza katika kongamano hilo, Ayatullah Araki alisema mhimili imara wa umoja wa Umma wa Kiislamu ni Ahul Bayt wa Mtume SAW na kuongeza kuwa: "Bibi Fatima Zahra SA ni mhimili wa Ahul Bayt Watoharifu AS.

Kwingineko akizungumza mjini Bombay, Ayatullah Araki alisema wenye itikadi za ukufurishaji wanalenga kuupokonya Uislamu nguvu zake. Amesema wakufurishaji walioenea aktiak ulimwengu wa Kiislamu wanataka Waislamu wafanya uadui na Mawalii wa Mwenyezi Mungu na wawe na urafiki na madui wa Mwenyezi Mungu. Amesema hii ndio sababu makundi ya Mawahhabi wakufurishaji hawana tatizo na utawala wa kizayuni wa Israel lakini wana uhasama wa wazi na wale ambao wanatetea mapambano ya taifa la Palestina.

Ayatullah Muhsin Araki aliwasili India Jumanne wiki iliyopita kwa lengo la kushiriki katika kongamano la"Umoja wa Umma katika Sira ya Bibi Fatima Zahra SA" ambapo pia anaonana na Maulamaa wa India.

3572336


captcha