IQNA

Magaidi wahujumu Kituo cha Qur'ani Idlib, Syria na kuua watu 7

13:01 - July 06, 2017
Habari ID: 3471053
TEHRAN (IQNA)-Magaidi wa wakufurishaji wamehujumu kwa mabomu Kituo cha Qur'ani katika mkoa Idlib kasskazini magharibi mwa Syria na kuua watu 8 na kuwajeruhi wengine 16.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, magaidi wao walifika na gari lililosheheni mabomu katika mlango wa Kituo cha Qur'ani (Darul Qur'an) katika mji mdogo wa Quneitra mkoani Idlib na kulipua bomu hapo ambapo raia 8 wameuawa shahidi.

Mkuu wa kamati ya kuulinda mji Mustafa Hajj Yusuf amesema miongoni mwa walipoteza maisha katika tukio hilo la kigaidi ni watoto waliokuwa wamefika katika kituo hicho kujifunza Qur'ani Tukufu.

Aidha amesema waliojeruhiwa wamefikishwa hospitali na kwamba baadhi wanakabiliwa na hatari ya kupoteza maisha. Hadi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililodai kuhusika na hujuma hiyo.

Magaidi wakufurishaji wa makundi ya ISIS au Daesh, Al Nusra n.k yamekuwa yakiendesha kampeni ya kinyama nchini Syria tokea mwaka 2011. Serikali ya Syria inasema magaidi wanapata himaya ya baadhi ya tawala za Kiarabu hasa Saudi Arabia na pia madola ya magharibi hasa Marekani.

3615656

captcha