IQNA

Uturuki kusambaza nakala za Qur'ani katika nchi 15 za Afrika

22:03 - October 28, 2017
Habari ID: 3471233
TEHRAN (IQNA)-Uturuki imeanza kusambaza nakala 21,500 za Qur'ani katika nchi 15 barani Afrika.

Taarifa zinasema nakala hizo za Qur'ani zinasambazwa kupitia Idara ya Waqfu katika mkoa wa Konya nchini Uturuki. Mpango huo wa kusambaza nakala hizo za Qur'ani umepewa jina la "Undugu wa Qur'ani Barani Afrika."

Igul Ardam, mkurugenzi wa wa Idara ya Waqfu ya Konya amesema mpango huo unalenga kuwasaidia wale wanaotaka kusoma Qur'ani barani Afrika.

Lori ambalo lilikuwa limebeba nakala hizo 21,500 za Qur'ani liliondoka Konya baada ya sherehe iliyofanyika mjini Konya. Idara ya Waqfu Uturuki inafungamana na Idara ya Masuala ya Kidini katika Ofisi ya Rais wa Uturuki maarufu kama Diyanet.

3657138
captcha